Utitiri wa maduka ya dawa tatizo
nchini
KWA UFUPI Watu wanapata madhara kutokana na
kukiukwa kwa taratibu za upatiwaji wa dawa unaofanyika zaidi katika maduka ya
dawa yasiyo na wataalamu Dar es Salaam. Chama cha Mafamasia nchini (PST)
kimesema matatizo mengi yatokanayo na matumizi mabaya ya dawa yanasababishwa na
uwepo wa maduka ya dawa yasiyo na wataalamu na yanayoendeshwa kiholela.
Akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Mafamasia nchini, Rais wa PST, Michael Kishua alisema Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani, inaendeshwa kwa misingi na sheria katika huduma za dawa lakini kuna utekelezaji hafifu wa sheria. “Sisi kama chama, tukiona kuna upungufu tunazungumza na baraza la famasia ili warekebishe na mpaka sasa tumeona kuna mabadiliko makubwa kwa sababu hata sasa baraza la famasia lipo kazini likiangalia maduka yanayoendeshwa kiholela,” alisema Alisema tabia ya watu kununua dawa kiholela bila ya kuwa na cheti cha maelekezo daktari hufanywa na maduka ambayo yanavunja sheria na yale yasiyo na wataalamu na kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji. Kadhalika, chama hicho kilikiri kuwa yapo maduka yanayouza dawa za kutoa mimba na kusisitiza kuwa mienendo hiyo inakemewa kwa pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Baraza la Mafamasia la Taifa. “Kigezo cha kwanza cha duka la dawa ni kusajiliwa na kuwa na wataalamu wa masuala ya dawa. Baraza la Mafamasia haliwezi kusajili duka bila kuwa na mtaalamu wa uhakika,” alisema Kishua. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa PST, Elias Masumbuko alisema ipo sheria inayofafanua dawa zinazotakiwa kununuliwa bila cheti na zile za moto zinazohitaji cheti lakini mara kadhaa sheria hiyo inakiukwa. Aliwataka wamiliki wa maduka ya dawa kutoweka mbele biashara badala yake wazingatie maadili ya taaluma ili kuepusha madhara. Wakizungumzia maadhimisho ya wiki hiyo ya mafamasia nchini inayofikia kilele chake leo, Kishua alisema ni vyema Watanzania wakaeleweshwa umuhimu wa kupata dawa kwenye vyanzo vinavyoaminika na salama. Alisema mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo ni Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donald Mbando ambaye pia atazindua tovuti ya chama hicho. Maadhimsho ya Wiki ya Mafamasia nchini kwa mwaka huu yanapambwa na kauli mbiu isemayo, ‘Elewa dawa zako, mfahamu famasia wako.’

Comments
Post a Comment