MAMLAKA
YA CHAKULA NA DAWA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
KUFUTA USAJILI
NA KUDHIBITI MATUMIZI YA BAADHI YA DAWA ZA BINADAMU
|
1. Mamlaka ya Chakula na Dawa ni wakala
wa Serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la
kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
2. Mamlaka imeweka mifumo mbalimbali
ya udhibiti ikiwa ni pamoja na mifumo ya tathmini na usajili, ukaguzi,
uchunguzi wa kimaabara, ufuatiliaji wa usalama wa dawa (pharmacovigilance) na ufuatiliaji
wa ubora wa dawa kwenye soko (post-marketing surveillance).
3. Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa
kupitia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa imebaini uwepo wa dawa
duni kwenye soko, zenye madhara na zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.
4. Kufuatia hali hiyo, Mamlaka imefuta
usajili wa aina tano (5) za dawa za binadamu kama ifuatavyo:-
Na.
|
Aina ya Dawa
|
Hatua iliyochukuliwa
|
Sababu za kuchukua hatua
|
i.
|
Dawa ya kutibu
“fungus” ya vidonge na kapsuli aina ya Ketoconazole
|
Kufuta usajili na
kuzuia uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi
|
Kusababisha madhara
hatarishi katika ini kwa watumiaji (liver toxicity)
|
ii.
|
Dawa ya kutibu
malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine (Monotherapy)
|
Kufuta usajili na
kuzuia uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi
|
·
Mabadiliko
ya Mwongozo wa Kisera wa Kupima na Kutibu Malaria wa mwaka 2013, Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii.
·
Amodiaquine
ikitumika peke yake (monotherapy) inaleta usugu wa vimelea vya malaria lakini itaendelea kutumika kama dawa ya mseto pamoja
na “Artesunate”.
|
iii.
|
Dawa za kutibu mafua
na kikohozi za maji, vidonge na kapsuli
zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanolamine
|
Kufuta usajili na
kuzuia uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi
|
Madhara hatarishi
kwa watumiaji kama vile kiharusi (hemorrhagic stroke)
|
iv.
|
Dawa ya kuua bakteria
ya sindano aina ya Chloramphenicol
Sodium Succinate inayotengenezwana kiwanda cha Lincoln
Pharmaceuticals Ltd, India
|
·
Kufuta
usajili na kuzuia uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi
·
Dawa
zenye kiambata hai aina ya Chloramphenicol za makampuni mengine zinafanyiwa tathmini
na ikibainika zina madhara zitaondolewa kwenye soko.
|
Madhara hatarishi
kwa watumiaji kama vile kushindwa kupumua na kupoteza fahamu (difficulty in
breathing and loss of consciousness)
|
v.
|
Dawa ya kuua bakteria ya maji na kapsuli
aina ya Cloxacillin
|
·
Kufuta
usajili na kuzuia uingizaji
·
Dawa
hii imeanza kuondolewa kwenye soko (phasing out)
|
Kiwango cha kiambato hai hupungua kabla ya muda wa
matumizi kumalizika (loss of potency before expiry date)
|
5. Vile vile, Mamlaka imebadili na
kudhibiti zaidi matumizi ya dawa nne (4) kama ifuatavyo:-
6. Kutokana na maamuzi haya, Mamlaka
inatoa maelekezo yafuatayo kwa watoa huduma za afya:
a.
Kuacha
kutoa kwa wagonjwa dawa zilizofutiwa usajili yaani Ketoconazole, Amodiaquine (inapotumika
yenyewe - monotherapy), Phenylpropanolamine
na Chloramphenicol Succinate Injection ya Lincoln Pharmaceuticals Ltd., India na
badala yake wazirudishe kwa wasambazaji wa dawa hizo.
b.
Kusimamia
mabadiliko ya matumizi ya dawa aina ya SP
ili ziweze kutumika kwa kinamama wajawazito tu na dawa aina ya Kanamycin, Amikacin na Levofloxacin zitumike kwa wagonjwa wa kifua kikuu tu
kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati.
c.
Kuendelea
kutoa dawa aina ya Cloxacillin hadi hapo
itakapomalizika kwenye soko kwa sababu matoleo (batches) yaliyopo yameshapimwa
na kuthibitishwa kuwa yanakidhi vigezo vya ubora.
7. Tunawahakikishia watoa huduma za afya
na wananchi kwamba kuondolewa katika soko kwa dawa zilizofutiwa usajili hakutaathiri
tiba kwa kuwa zipo dawa mbadala zinazoweza kutibu magonjwa yanayotibiwa na dawa
hizi.
8. Tunawakumbusha watengenezaji na
wasambazaji wa dawa kuhakikisha kwamba wanatengeneza dawa zinazokidhi vigezo
vya usalama, ubora na ufanisi kwa mujibu
wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi,
Sura 219. Wale wote watakaobainika
kuingiza na kusambaza dawa zilizofutiwa usajili watachukuliwa hatua kali za
kisheria.
9. Tunawashukuru watalaam wa afya na
wananchi kwa ujumla kwa kuendelea kutoa taarifa za madhara na ubora wa dawa zilizo
kwenye soko kwani kwa kufanya hivyo wananchi watajikinga na madhara yatokanayo
na matumizi ya dawa na kuwa na afya njema.
10. Tunawashukuru wanahabari kwa ushirikiano mkubwa
ambao mmekuwa mkiuonesha katika kutoa taarifa zinazohusu masuala ya udhibiti wa
ubora na usalama wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba na tunaomba
muendeleze ushirikiano huo.
Imetolewa na;
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Chakula na Dawa,
S.L.P 77150,
Dar es Salaam.
Simu: +255 22 2452108/2450512/2450751/658 445222/777 700 002
Nukushi: +255 22 2450793
Baruapepe: info@tfda.or.tz
Tovuti: www.tfda.or.tz
Comments
Post a Comment