Skip to main content

KUFUTA USAJILI NA KUDHIBITI MATUMIZI YA BAADHI YA DAWA ZA BINADAMU



MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


KUFUTA USAJILI NA KUDHIBITI MATUMIZI YA BAADHI YA DAWA ZA BINADAMU


1.    Mamlaka ya Chakula na Dawa ni wakala wa Serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2.    Mamlaka imeweka mifumo mbalimbali ya udhibiti ikiwa ni pamoja na mifumo ya tathmini na usajili, ukaguzi, uchunguzi wa kimaabara, ufuatiliaji wa usalama wa dawa (pharmacovigilance) na ufuatiliaji wa ubora wa dawa kwenye soko (post-marketing surveillance).

3.    Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa kupitia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa imebaini uwepo wa dawa duni kwenye soko, zenye madhara na zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

4.    Kufuatia hali hiyo, Mamlaka imefuta usajili wa aina tano (5) za dawa za binadamu  kama ifuatavyo:-

Na.
Aina ya Dawa
Hatua iliyochukuliwa
Sababu za kuchukua hatua
i.
Dawa ya kutibu “fungus” ya vidonge na kapsuli aina ya Ketoconazole
Kufuta usajili na kuzuia uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi
Kusababisha madhara hatarishi katika ini kwa watumiaji (liver toxicity)
ii.
Dawa ya kutibu malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine (Monotherapy)
Kufuta usajili na kuzuia uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi

·         Mabadiliko ya Mwongozo wa Kisera wa Kupima na Kutibu Malaria wa mwaka 2013, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
·         Amodiaquine ikitumika peke yake (monotherapy) inaleta usugu wa  vimelea vya malaria lakini  itaendelea kutumika kama dawa ya mseto pamoja na “Artesunate”.
iii.
Dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanolamine

Kufuta usajili na kuzuia uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi
Madhara hatarishi kwa watumiaji kama vile kiharusi (hemorrhagic stroke)
iv.
Dawa ya kuua bakteria ya sindano aina ya Chloramphenicol Sodium Succinate inayotengenezwana kiwanda cha Lincoln Pharmaceuticals Ltd, India
·      Kufuta usajili na kuzuia uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi

·      Dawa zenye kiambata hai aina ya Chloramphenicol za makampuni mengine zinafanyiwa tathmini na ikibainika zina madhara zitaondolewa kwenye soko.

Madhara hatarishi kwa watumiaji kama vile kushindwa kupumua na kupoteza fahamu (difficulty in breathing and loss of consciousness)
v.
Dawa ya kuua bakteria ya maji na kapsuli aina ya Cloxacillin
·      Kufuta usajili na kuzuia uingizaji

·      Dawa hii imeanza kuondolewa kwenye soko (phasing out)
Kiwango cha  kiambato hai hupungua kabla ya muda wa matumizi kumalizika (loss of potency before expiry date)

5.    Vile vile, Mamlaka imebadili na kudhibiti zaidi matumizi ya dawa nne (4) kama ifuatavyo:-

Na
Aina ya Dawa
Hatua iliyochukuliwa
Sababu za kuchukua hatua
i.
Dawa ya kutibu malaria ya vidonge yenye mchanganyiko wa Sulphadoxine na Pyrimethamine(SP)
·       Kubadili matumizi kutoka tiba ya malaria na kuwa kinga ya malaria kwa kinamama wajawazito

·       Watengenezaji wamejulishwa na wamebadili lebo za dawa hizo


Mabadiliko ya Mwongozo wa kisera wa Kupima na Kutibu Malaria wa mwaka 2013, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

ii.
Dawa aina ya Kanamycin, Amikacin na Levofloxacin
Kudhibiti matumizi kwa kuruhusu dawa hizi kutumika kwa ajili ya ugonjwa wa kifua kikuu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati tu
Kuzuia usugu wa vimelea vya bakteria
vya ugonjwa wa kifua kikuu

6.    Kutokana na maamuzi haya, Mamlaka inatoa maelekezo yafuatayo kwa watoa huduma za afya:

a.            Kuacha kutoa kwa wagonjwa dawa zilizofutiwa usajili yaani Ketoconazole, Amodiaquine (inapotumika yenyewe - monotherapy), Phenylpropanolamine na Chloramphenicol Succinate Injection ya Lincoln Pharmaceuticals Ltd., India na badala yake wazirudishe kwa wasambazaji wa dawa hizo.

b.            Kusimamia mabadiliko ya matumizi ya dawa aina ya SP ili ziweze kutumika kwa kinamama wajawazito tu na dawa aina ya Kanamycin, Amikacin na Levofloxacin  zitumike kwa wagonjwa wa kifua kikuu tu kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati.

c.            Kuendelea  kutoa dawa aina ya Cloxacillin hadi hapo itakapomalizika kwenye soko kwa sababu matoleo (batches) yaliyopo yameshapimwa na kuthibitishwa kuwa yanakidhi vigezo vya ubora.

7.    Tunawahakikishia watoa huduma za afya na wananchi kwamba kuondolewa katika soko kwa dawa zilizofutiwa usajili hakutaathiri tiba kwa kuwa zipo dawa mbadala zinazoweza kutibu magonjwa yanayotibiwa na dawa hizi.

8.    Tunawakumbusha watengenezaji na wasambazaji wa dawa kuhakikisha kwamba wanatengeneza dawa zinazokidhi vigezo vya  usalama, ubora na ufanisi kwa mujibu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219.  Wale wote watakaobainika kuingiza na kusambaza dawa zilizofutiwa usajili watachukuliwa hatua kali za kisheria.

9.    Tunawashukuru watalaam wa afya na wananchi kwa ujumla kwa kuendelea kutoa taarifa za madhara na ubora wa dawa zilizo kwenye soko kwani kwa kufanya hivyo wananchi watajikinga na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa na kuwa na afya njema.

10.  Tunawashukuru wanahabari kwa ushirikiano mkubwa ambao mmekuwa mkiuonesha katika kutoa taarifa zinazohusu masuala ya udhibiti wa ubora na usalama wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba na tunaomba muendeleze ushirikiano huo.






Imetolewa na;

Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Chakula na Dawa,
S.L.P 77150,
  Dar es Salaam.
Simu: +255 22 2452108/2450512/2450751/658 445222/777 700 002
Nukushi: +255 22 2450793
Baruapepe: info@tfda.or.tz

Comments

Popular posts from this blog

carrier path event on 17th june 2015

prof KENNEDY MWAMBETE   Ms.   E l izabeth   Shekala g he,   R e gis t rar pharmacy council  giving speech through Skype  front seat PROF KAALE{LEFT} ,SILO, Mr GEORGE,Issa, Mr   A nant   Bhalani   Mr.   George   Lugat a ,   T er r i t or y   manager   T i g o  Students and other stuff members listening to speeches  dean School of Pharmacy Prof Veronica Mgoyela CHAIR MAN SCHOOL OF PHARMACY PIUS DANIEL KIWANGO {Wth neck tie} PROF KAALE   Discussions/Que s tions   a nd   Answers   Mr.   H i i t i   S il o ,   D G   TFDA  responding to questions from students  Tumain Makole asking question  Jesse bpharm4 aking questions

NATIONAL PHARMACY WEEK 14th-20th JUNE 2015

PHARMACEUTICAL ASSOCCIATION OF TANZANIA NATIONAL PHARMACY WEEK 14 TH - 20 TH JUNE 2015 Theme Self-medication: How safe? Ask your Pharmacist PROGRAM FOR TAPSA PARTICIPATION 19 TH at MLIMANI CITY, MAKUMBUSHO AND KIVUKONI 20 TH at MNAZI MMOJA Come to our tents and get free advice FREE TRANSPORT, MEALS AND DRINKS WILL BE PROVIDED DON’T DARE TO MISS IT Self-medication self-medication is defined as "the use of drugs to treat self-diagnosed disorders or symptoms, or the intermittent or continued use of a prescribed drug for chronic or recurrent disease or symptom Or is a human behavior in which an individual uses a substance or any exogenous influence to self-administer treatment for non-clinical physical or psychological ailments.

ABOUT TAPSA

Being the student aspiring to be health cadre delivers and service providers we are entitled responsibility to the Tanzanians and world at large as tomorrow health practitioners. Having a goal to prepare diligent health professionals ADUPS was founded in Mid August 1987 by MUCHS pharmacy students and as a result of guidance and support from IPSF, the association was officially registered on the 4th April 1990 in UDSM.  It became a full member of IPSF and APSF in August 1993 and September 2002 respectively.  ADUPS has being active for almost twenty years and her members have every reason to be proud for attaining this age. In the year-2007 MUCHS declared transformation from being a constituent College of University of Dar es Salaam to full fledged University hereby namely MUHAS. ADUPS had to transform her name and become TAPSA.  Following this expansion the association is having chapters in Colleges/Universities providing a bachelor of P...